Msanii mkongwe katika game la muziki wa kizazi kipya, an icon, Temeke native, Juma Nature, ni moja ya wasanii waliotokea kupendwa sana nchini Tanzania, Juma Kassim Nature a.k.a Kiroboto ameweza kumantain game na kuendelea kuwa msanii anayependwa ingawa hajatengeneza hit siku nyingi.
“mimi ni bidhaa tayari, tena yenye ubora, toka gari aina ya benz ilipotengenezwa zimetengenezwa gari nyingi lakini benz imeendelea kupendwa na kuonekana ni gari bora, ila limekuwa likiboreshwa tu, hata lisipotangazwa lakini linajulikana tayari, kwa hiyo mimi ni kama benz, nimefanya kazi nzuri siku za nyuma you can’t take that from me, nilishatangzwa mwanzo nikafanya vizuri, wengine lazima waje lakini nao ni bidhaa nyingine, mimi benz, wao wanaweza kuwa, Ferrari, Cadillac, Lamborghini, Mclaren, Toyota mark x kwa hiyo kila bidhaa na watu wake na ubora wake, kwa hiyo mimi kupendwa ni kupendwa tu” amesema.
Pia Nature amepost kupitia instagram akiwa na Mhe. Edward Lowassa na kuandika “Mungu yunasi mloshindwakunitumia kikazi msinilaumu”. maneno haya ya Nature inavyoonekana ameyaelekeza kwa wote wanaomchukulia poa wakidhani ameshuka kimuziki na hivyo kuacha kufanya nae kazi na inavyoonekana atakuwa amepewa kazi na Mhe. Lowassa anaweza akawa nae endapo atateuliwa kugombea urais kupitia Chadema baada ya kuchukua fomu siku ya jana.
Kwa maana hiyo Nature atakuwa moja ya wasanii watakaofanya kazi ya kampeni wakiwa na Mhe. Edward Lowassa katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.