Mtu mmoja amenusurika kufa baada ya gari alilokuwa akiendesha aina ya Land Cruiser hard top kusombwa na mafuriko katika eneo la kijiji cha Mererani wilayani Karatu barabara kuu ya Karatu Arusha.
Manusura huyo dereva wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro aliyekua akiendesha gari yenye namba za usajili SU 36037 na kutambuliwa kwa jina la Juma Moshi ameokolewa na wasamaria wema ambao walifanikiwa kumnasua kutoka juu ya mti aliokua amepanda na kujisitiri kwa takribani saa nzima na kuwahishwa hospitali kwa uchunguzi wa afya yake.
Wakati huo huo mafuriko hayo yamekwamisha mamia ya abiria waliokua wakisafiri kutoka karatu kwenda Arusha na Arusha kwenda Karatu kwa muda wa zaidi ya saa tano baada ya daraja la mto Kirurumo jirani na mji mdogo wa mto wa Mbu kufunikwa kwa maji na mawe .
Akizungumza katika eneo la tukio ambapo hata hivyo baada ya mawe kupunguzwa magari yaliendelea na safari mkuu wa wilaya ya Karatu Daudi Ntibenda anakiri eneo hilo kuwa tatizo na kwamba serikali iko kwenye hatua za kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Hali Ilivyokuwa