Polisi wa New York wanamtafuta mwanamke Wakimarekani mwenye asili ya Afrika ambaye alionekana akimsukuma mtoto wake kutoka kwenye treni.
Taarifa kutoka Daily Mail zinasema, shuhuda mmoja aliona mwanamke mmoja Mmarekani mwenye asili ya Afrika akikadiriwa kuwa na miaka 20 hadi 30 akisukuma basikeli cha watoto (Stroller) kutoka kwenye treni huko Columbus muda wa saa 11:50 asubuhi.
Mwanamke huyo baada ya kumuacha mtoto huyo alirudi kwenye treni kabla milango haijafunga nakumacha mtoto aliyekadiriwa kuwa na umri wa miezi 7 akiwa mwenyewe. Video iliyonaswa na kamera ilitolewa na NYPD inamuonyesha mwanamke huyo akiingi kwenye njia za chini za treni akiwa anamsukuma mtoto huyo mapema siku hiyo.
Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 33 aliyekuwa amesimama hapo alimuona mtoto huyo alikaa nae kwa dakika 20 akisubiri mama yake arudi lakini hakuna mtu yeyote aliyerudi kumtafuta mtoto huyo, mashuhuda waliokuwapo eneo la tukio waliwapigia simu pilisi.