
Mkazi mmoja wa Temeke Kota jijini Dar es salaam aliyefahamika kwa jina la Bib Jilahalae amegoma kuhama kwenye nyumba ambayo inatakiwa kuvunjwa katika eneo hilo ili kupishaujenzi wa mradi mkubwa wa uwekezaji akidai kuwa hajatendewa haki katika mchakato mzima wa zoezi na kusisitiza kuwa hatoondoka na yuko tayari nyumba ivunjwe akiwa ndani.
hata hivyo bibi huyo amesema hayuko tayari nyumba yake kubomolewa kwani hapana pa kwenda.
hata hivyo baadhi ya majirani wametupia lawama serikali na kusema serikali inatakiwa kumwangalia bibi huyo na kumtafutia mahala pa kuishi na kuacha kutumia nguvu za kumwondoa..,
