
Ikiwa imesalia timu moja tu ya Afrika ambayo angalau inaleta tumaini kwa kushinda mchezo wake wa ufunguzi, Ivory Coast ambayo inashuka leo uwanjani kuivaa timu kutoka bara la Marekani ya kusini Colombia, timu nyingine za Afrika imekuwa ni kilio ambapo jana tulishuhudia Cameroon akichakazwa 4 akichakazwa 4 – 0 na Croatia.
Mechi nyingine ya jana ilikuwa ni Hispania bingwa mtetezi ambae alichakazwa 2 – 0 na Chile hivyo kuvunja matumaini yake ya kusonga mbele katika kombe la dunia Brazil 2014.
Australia nae akapigwa 3 – 2 na Uholanzi katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.
Leo Uruguay inashuka dimbani kuikabili Uingereza aliyejeruhiwa na Italia katika mechi ya ufunguzi, Japan nae atakuwa akiivaa Ugiriki katika mchezo unaotegemewa kuwa mkali sana.
Afrika inashuka Ivory Coast kuivaa Columbia pia katika mchezo unaotegemewa kuwa mkali siku ya leo. Kesho Ijumaa 20 Juni 2014 Italia itavaana na Costa Rica, Switzeland itaivaa Ufaranza na Honduras itaivaa Ecuador.
