Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya nchini Kenya imeagiza kuchunguzwa kwa fomu 34 za matokeo ya uchaguzi wa rais kutoka katika vituo vyote 34,400, vilivyotumika kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Machi 4, mwaka huu.
Kadhalika mahakama hiyo jana iliagiza kuhesabiwa upya kwa kura za urais katika vituo vya kupigia kura 22 kati ya elfu 33 vilivyolalamikiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Muungano wa Cord, Raila Odinga.Katika malalamiko yake yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo kupinga Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Machi 4, Odinga alidai kuwa vituo hivyo 22 kura zilizopigwa zinazidi idadi ya wapigakura walioandikishwa.Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya majaji wenzake watano, Jaji Smokin Wanjala alisema kwamba uhesabuji kura wa vituo hivyo utafanyika leo kuanzia saa 2.00 asubuhi kwa lengo la kubaini ukweli kuhusu madai hayo.
Matokeo ya Urais Kenya Kuhesabiwa Upya.
Previous Story
Q Chila Na Shilole Kuitingisha Mwanza Siku Ya Pasaka
Next Story
Angelina Jolie Akiwa Congo DRC [Video]
Related Posts
-
-
picha: Naomi Campbell, Bono, Jacob Zuma na wake za Mandela Winnie na Graca watoa heshima za mwisho kwa Nelson Mandela
-
Rihanna Na Lewis Hamilton Waongeza Mafuta Kwenye Moto Wa Uvumi Kuwa Ni Wapenzi
-
Chriss Brown Apatikana Na Kosa La Shambulio Aomba Msamaha
-
Makamu Wa Rais Dr. Bilali Aongoza Mamia Maziko Ya Mwaamuziki Gurumo
-
Simon Cowell Haoni One Direction Wakirudi Baada Zayn Malik Kujitoa
-
Historia Imeendelea Kuitesa Uholanzi Katika Kombe La Dunia