
Ukitaka kujua kwanini nimesema hivyo ni baada ya kuona picha kupitia ukurasa wa instagram wa mtu fulani hivi, kanye West akiwa na hasira na jinsi anavyofanya vitu ni kama mjinga anapokuwa na Kim.
Kijana huyo alisema Kanye West amepoteza heshima yake kwenye dunia ya rap sio kwa sababu alimuoa Kim K lakini ni kwa sababu anafanya vitu vya kijinga kama anamuabudu Kim K.
Kila wakati yuko nyuma yake, akisukuma wahandishi wa habari, akimfungulia mlango na kumtengeneza nguo kama yeye ni mfanyakazi wake.
Wanawake walikuwa wakitoa maoni yao wakisema kwamba hivyo ndivyo mwanaume wa kweli anatakiwa kumfanyia mwanamke wake kwenye umati wa watu.
Anaonyesha heshima kwa Kim Kardshian na jinsi anavyomhudumia kwa heshima.
Kabla ya kuwa na Kanye West, Kim K alikuwa mtu fulani tu wa kawaida kwa sababu hakuna mtu alikuwa akimualika sehemu kivile. Alikuwa akihost club parties lakini yote hayo yamechange amekuwa queen, popote anapotokea Kim K duniani lazima ajaze watu kinoma noma, juzi kati huko Paris watu walisukumana kidogo mtu mmoja amuangushe mrembo huyo.
Nadhani Kanye West ametekwa na Kim, lakini kwa sababu kutekwa huko hakuhatarishi maisha yake ni mahaba niue, ni sawa kabisa…lakini nani anapenda jinsi anavyomfanyia Kim K wakiwa kwenye public? Kuna vitu vingine kama mwanaume alafu mko kwenye umati unapotezea….
