
Hon James Macharia
Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto wamechagua kabinet ya mawaziri ambao wataunda timu itayoongoza serikali yao mpya ya jubilee na wametangaza baadhi tu ya majina ya mawaziri hao wapya.
Dr Fred Matiangi Okengo amechaguliwa kama waziri wa Wizara ya Mawasiliano Technolojia na Habari ya nchi hiyo, Henry K Rotich katika Hazina, James Wainanina Macharia amechaguliwa kuiongoza wizara ya Afya na Balozi Amina Mohammed amechaguliwa kama waziri wa wizara ya mambo ya nnje, Majina mengine 14 yatatangazwa pale mambo yatakapokuwa tayari.
Wizara nchini kenya zimepunguzwa kutoka viti 44 mpaka kufikia 18 kwa sasa.
Hon. Fred Okengo
Hon Amina Mohammed
Hon. Henry Rotich
