Bingwa wa dunia katika masumbwi mkali Mayweather amesema jinsi anavyompenda Justin Bieber haiwezi kuelezeka baada ya Bieber kuwasaidia watoto wa Mayweather katika ajali mbaya iliyotokea ikihusisha watoto wake. Akitoka kwenye duka la pombe huko Hollywood Jumatatu usiku hakusita kutoa ya moyoni juu ya Justin Bieber kwa ukarimu wake aliouonyesha kwa watoto wake watatu, alifunguka hayo alipokutana na kamera ya TMZ.
Siku hiyo Mayweather alikuwa kwenye red carpet ndipo alipopewa taarifakwamba watoto wake wamepata ajali, ndipo alipompigia Bieber na akaelekea eneo la tukio kutoa msaada na aliwachukua.
Justin Bieber aliwaambia askari kwamba yeye alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia hiyo akiwa na gari yake aina ya SUV, ajali ilitokea Los Angeles, taarifa zinasema ni gari mbili ziligongana.
Watoto wa MAyweather hawakuumia sana, mmoja alipasuka mdomoni kwenye lip, Justin Bieber katika kuwafariji aliwasikilizisha ngoma yake mpya, baada ya kuruhusiwa kuwachukua na akawapeleka kwa baba yao na alirudi katika eneo la ajali akawaambi polisi kwamba amewapeleka kwa baba yao. Hapa sikiliza Mayweather anavyompa shouts Justin Bieber.