Mauzo ya albamu sio kila wakati yanakuwa ni kigezo, lakini namba zinasaidia kujua ni nani anafanya vizuri mainstream. Level, Rick Ross anaheshima ya kuwa moja ya rappers ambao juu katika game la Hip Hop baada ya albamu zake kukamata namba 1 kwa miaka 10 iliyopita.
Lakini je Rozay amepitwa na vijana wake Meek Mill na Wale aliowasaini chini ya MMG yeye akiwa boss?
Wote watatu waliachia albamu zao mwaka huu,na Ijumaa iliyopita tarehe 4 Rozay aliachia albamu yake ya 8 inayoitwa “Black Market” na kutokana na makadirio ya mwanzo anategemea kuuza copies 50,000 na 55,000 katika wiki ya kwanza. Mastermind ya Rick Ross iliuza copies 179,000 kwenye wiki yake ya kwanza mwaka 2014 na baadae albamu ya “Hood Millionaire” iliuza copies 74,000 ndani ya siku 7.
Mwaka mmoja baadae Rick Ross anashuka kimauzo na kuwa chini ya Mee na Wale, Albamu ya Wale ya About Nothing88,000 iliuza copies na kushika namba katika charts za Billboard 200.
Miezi 3 baadae Meek Mill aliachia albamu inayoitwa “Dreams Worth More Than Money” ambayo iliuza copies 215,000 katika wiki yake ya kwanza. Albamu hiyo ya rapper huyo kutoka Philladelphia ilikaa namba 1 kwenye charts kwa wiki 2, alikuwa ni ya wasanii wa Hip Hop waliouza zaidi ya copies 200,00 katika wiki ya kwanza mwaka 2015, waliofanya hivyo ni pamoja na Drake, Future,Kendrick Lamar na Dr.Dre.
Mwaka unaisha,Je mwaka utaisha wanafunzi wanampita mwalimu kwa kujulikana na kuwa na watu wengi zaidi? M M G camp wamejipanga kuachia mixtape ya Self Made ya Rozay, na Meek Mill amekuwa akikamilisha mixtape yake ya Dreamchasers 4.
Meek Mill Na Wale, Wanafanya Vizuri Zaidi Kuliko Boss Wao Rick Ross?
08 December 2015 by Salma Msangi+ in
Entertainment News International Entertainment music Xpress News
- No Comments
Related Posts
-
-
Wadau wa muziki kukutana LEO Leaders Club kwaajili ya mipango ya kuisaidia familia ya Marehemu Mangwea
-
Pentagon Shopping Center wakongwe wa Mavazi ya officine na mitoko kwa ajili ya akina baba na kina mama wenye hadhi zao.
-
Baba Wa Beyonce Mr Knowles Azaa Na Mwanamitindo Muonyesha Nguo Za Ndani DNA Imethibitisha Kwa 99.998%
-
Urembo Na Malengo, Hongera Hoyce Temu kwa Kuwa Mfano Mzuri Kwa Warembo
-
Mwanamieleka Sean O’Haire, Star Wa Zamani Wa WCW Na WWE Ajinyonga
-
Breaking News: Bi Kidude Afariki Dunia