
Miley Cyrus amekuwa ni mwanadada mwenye vituko, unaweza ukamuweka katika kundi la kina Rihanna, Lady Gaga na wengine wenye vituko kama yeye, kwa kweli Cyrus amezidi kuwa na vituko, alishawahi kuwasha bangi akiwa stejini, pia hupenda kuvaa karibia na uchi akiwa sehemu mbalimbali.
Katika New York Fashion week mwanada huyo amewaacha watu midomo wazi baada ya kutokea pale Alexander Wang katika after party ya New York Fashion akiwa topless ila akiwa ameziba chuchu tu huku akiwa na washkaji zake na walienjoy usiku huo wote.
Hakuna mtu aliyekuwa anasikia aibu na Cyrus mwenyewe alikuwa na furaha sana hana tatizo na mtu. Lakini baba yake baba yake Bill Ray lazima moyo uwe unamuuma hila ndo hakuna cha kusema, mtoto ana mkwanja wake ndo anakuweka mjini na vituko vyake, wewe kama baba ungemwambiaje?
Kama ice cream cone zilikuwa zimeficha chuchu zake tu sehemu nyingine zote za juu akiwa wazi akizunguka zunguka kwenye jengo la Alexander Wang kwenye after party ya New York fashion week.
Miley Cyrus siku hiyo alikuwa na Tyga, Kendall na Kylie Jenner na watu wengine, lakini watu wengine nje ya hao stories zinasema kwamba hawakupendezwa na kitendo hicho.
Ila kwa usiku ule Miley Cyrus ndo alikuwa kick katika after party kila mtu akimtazama na kumuongelea.
