Ingawa ugomvi wa Meek Mill na Wale umeendelea wiki chache zilizopita, akiongelea ugomvi huo wa Meek Mill na Wale , The Boss wa MMG Rick Ross amesema ugomvi huo tayari uliisha ulikuja na kuondoka.
Aliongelea ugomvi huo hasa pale Wale alipotoa maoni yake kuhusu ugomvi wa Meek Mill na Drake,katika mahojiano yaliyofanyika juzi kati na AllHipHop.com Rozay aliongeza wawili hao watakuwa brothers forever na siku moja watakuwa sehemu ambayo watatazama yale waliyopitia na kujifunza.
Akiongeza akiwalinganisha ugomvi wa Meek Mill na Drake alisema itatoka kwenye kalamu mpaka kwenye bunduki , Wale aliweka wazi kwamba MMG haipo pamoja kama ilivyokuwa kabla.
Tukiachana na ugomvi huo, albamu mpya ya Rick Ross inayoitwa “Black Market” imepangwa kutoka Desemba 4, Rozay alitoa taarifa hizo wakati wa mahojiano hayo.
Albamu hiyo itakuwa na ngoma ambazo zitakuwa na miondoko ya Soulfull, hapa utamsikia Rozay ambae anajimwaga kwenye beats za live music.
Angalia video ya mahojiano hapo chini: