Baada Ya tukio La kupotea kwa Mrembo wa Honduras Miss Honduras Aliyetakiwa kushiriki mashindanoya miss world yanayoendelea sasa huko london, Mpenzi wa Dada yake mkubwa miss honduras Sophia Trinidad ndio anayesadikiwa kuwauwa mrembo huyo na dada yake
Plutarco Ruiz kwenye picha (upande wa kulia) amekubali kuwa anahusika na mauaji ya mpenzi wake Sophia,23, baada ya kumuona anacheza muziki na mwanaume mwingine katika sherehe ya sikukuu yake ya kuzaliwa na hapo ndio ulikuwa mwisho wa sophia na baada ya hapo aliendelea na mauaji hayo kwa mdogo mtu wa sophia ambaye ni miss Honduras 2014 maria Jose Alvarado eti kwasababu alishuhudia mauaji ya Dada yake
Wanaume wengine watatu wamekamatwa kutokana na Tukio Hilo
baada ya kuwauwa waliwazika katika eneo la RiverBank karibu kabisa na mauaji yalipofanyika
Ruiz akiwa amewapeleka police kuwaonyesha eneo alilowazika wanawake hao,