Mkenya Wilson Kipsang amevunja rekodi ya dunia ya mbio za Marathon kwa kupunguza sekunde 15 aliposhinda mbio za Berlin mapema jumapili.
Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 31 aliandikisha mda wa saa mbili dakika tatu na sekunde 23 kuondoa rekodi ya zamani iliyowekwa na Mkenya mwenzake Patrick Makau miaka miwili iliyopita.
Rekodi hiyo iliwekwa katika mji mkuu wa Ujerumani ambako Makau alikimbia kwa mda wa saa 2:dakika 03:na sekunde 38.
Wakenya wengine walioshiriki mbio a Berlin Eliud Kipchoge alimaliza katika mda wa saa 2:04:05) huku Geoffrey Kipsang akiweka mda wa saa 2:06:26 katika nafasi ya tatu.
Makau hakushiriki mbio hizi baada ya kujiondoa wiki mbili zilizopita kutokana na kuuguza jeraha la goti.