Muimbaji mkongwe wa Rock, David Bowie amefariki baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu, mkongwe huyo alifariki akiwa amelala. Kutokana na taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wake wa face book, David Bowie alifariki kwa amani leo akiwa amezungukwa na familia yake baada ya ujasiri waliouonyesha kwa miezi 18 akiugua saratani.
Wakati huu watu wengi watashare kuhusu kumpoteza David Bowie, watu wameombwa kuheshimu mambo binafsi ya kifamilia katika kipindi hiki cha huzuni.
Bowie ameacha watoto wawili na mke wake Iman ambae walioana toka Aprili 24, 1999.