C.E.O wa kampuni ya Apple Tim Cook, ameweka wazi rasmi kuwa yeye kuwa ni shoga, amesema anajivunia kuwa shoga.
Tim Cook aliyasema hayo kwa ajili ya kuwasaidia watu wanaong’ang’ania kuweka wazi jinsia zao katika ripoti iliyochapishwa katika gazeti la biashara la kila wiki Bloomberg.
Tim Cook alisisitiza katika jimbo la Alabama kuhakikisha haki za mashoga na wanaobadili jinsia waheshimiwe.
”Mimi sijitambui kama mwanaharakati,lakini nimegundua nilivyofaidika na mikakati iliowekwa na wengine”,alisema bwana Cook.
Tim Cook amesema ameweka wazi kuhusu ushoga na watu wengine wakiwemo wafanyakazi wenzake ndani ya kampuni hiyo, lakini haikuwa rahisi kufanya hivyo.
” Watu wakisikia kwamba mimi ni shoga itakuwa msaada kwao,au kumpa faraja yule anayejisikia kutengwa au kuwashinikiza wengine kupigania haki zao,basi afadhali kutangaza maisha yangu ya faragha”aliongezea.