Mkuu mpya wa wilaya ya Kinondoni PAUL MAKONDA aliyeteuliwa na Rais JAKAYA KIKWETE kushika wadhifa huo hivi karibuni na kupingwa na
baadhi ya watu huku wengine wakihoji uwezo wake kiutendaji, ameapishwa leo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam SAID MECK SADICK. Baada ya kula kiapo MAKONDA amesema atatekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kushirikiana na watendaji wengine kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora kama inavyohitaji Serikali iliyopo madarakani. Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam SAID MECK SADICK amesema kuteuliwa kwa Makonda kushika wadhifa huo kumekuja kwa wakati na kumtaka kusimamia usawa katika utekelezaji wa majukumu yake. MAKONDA ndiye mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa kipolisi Kinondoni ambaye ameahidiwa ushirikiano kiutendaji na Kamanda wa polisi wa mkoa huo CAMILLIUS WAMBURA anayezibainisha changamoto za kiusalama kinondoni. Wilaya ya Kinondoni ina jumla ya watu milioni 1.8 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012.