
Msanii wa Hip hop Tanzania Afande Sele Afiwa na mama mtoto wake anayefahamika kwa jina la Asha, Asubuhi ya kuamkia August 14 2014, Afande Sele aliweka ujumbe kuhusu taarifa hizi
Ndugu zangu!! Nimefiwa na Mzazi mwenzangu (Asha) /mama wa wanangu (mama Tunda/Mama Sanaa) ..ni pigo kubwa kwangu na wanangu. SISI NI WAJA WA MWENYEZI MUNGU NA HAKIKA KWAKE TUTAREJEA; MUNGU AMPUMZISHE PEMA.
Ujumbe huu uliambatana na Hii picha ya familia yake.
Kabla ya kifo chake Afande alifarakana na mke wake na walikuwa wakiishi sehemu tofauti, wana watoto wawili Tunda ambaye yuko kidato cha pili na Sana mwenye miaka 2.
Msiba upo Morogoro Mtaa wa Amani kwa Wazazi Wa Asha Mohhamed Shengo. Asha amezaliwa May 21 1981, Aliishi na Afande kwa miaka 16,Afande Sele amesema Asha aliugua malaria siku moja kabla ya kifo chake. Mungu akupe nguvu Afande Sele kipindi hiki kigumu..R.I.P Asha.
