Mwanamuziki wa kike wa nchini Kenya, Linet Munyali aka Size 8ametangaza kuachana na muziki wa dunia baada ya kuokoka.
Kuanzia sasa msanii huyo atakuwa akiimba nyimbo za injili napia ameshaachia video ya wimbo wake wa kwanza wa gospel, Meteke.
Size 8 ni msanii mwenye mafanikio makubwa nchini Kenya na amekuwa akitafutwa zaidi kufanya show kuliko msanii mwingine wa kike nchini humo. Ukimtoa Avril, hakuna msanii mwingine wa kike aliyeweza kushindana naye.