Msanii wa kibao maarufu cha Ashawo, Flavour wa nchini Nigeria ambaye hivi sasa ameibuka na kichupa kipya alichoshirikishwa na msanii Iyanya kinachoitwa ‘Jombolo’, hivi sasa amejipanga kufanya ziara ya kimuziki nchini Marekani itakayoanza kulipuka mnamo mwezi Julai mwaka huu.
Flavour N’abania ameelezea kuwa amekuwa kimya muda akijipanga vyema na ziara hiyo kubwa ambayo tayari ameweka ratiba nzima ambayo ataanza kutumbuiza na bendi yake mjini Dallas Texas, Houston Texas, Maryland na mwisho wa ziara hiyo itakuwa tarehe 13 mwezi huo wa July jijini New York.
Nae Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye nyota yake inaendelea kungara kila kukicha, Ommy Dimpoz anatarajia kufanya ziara kubwa huko nchini Marekani, ambayo imepewa jina Nai Nai USA tour ambayo itaanza rasmi kuanzia mwezi wa 9 mwaka huu.
Katika ziara hii, Ommy Dimpoz atafanya onyesho lake la kwanza kabisa huko Washington DC Septemba 21, likufuatiwa na onyesho jingine Boston tarehe 28 Septemba, kabla ya kuelekea Chicago ambapo atafanya onyesho Oktoba 5, na kufanya onyesho lingine huko Houston Octoba 12 na kumalizia huko Carlifonia tarehe 19 mwezi huo huo wa Octoba.
Ziara hii ni hatua nyingine kubwa kwa msanii Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa pia mbali na kuwa na rekodi kali katika vituo mbalimbali, pia anashikilia rekodi ya kuwa mshindi wa tuzo kadhaa kutoka Kilimanjaro Music Awards kwa mwaka huu.