“Huu ulikuwa uamuzi mgumu sana ambao nimeshawahi kuufanya, lakini ndo muda wa kuendelea mambo mengine, ni muda wa kukua na kukutana na changamoto nyingine katika njia nyingine” Aliandika Angie Martinez kwenye ukurasa wake wa Instagram jana Juni 18, 2014 “Nashukuru sana kwa muda wote niliokuwa na familia ya Emmis na kampuni na katika njia isiopimika imetengeneza maisha yangu.
Tumetengeneza historia pamoja kwa njia nyingi, zitaishi kichwani kwangu kumbukumbu zote na urafiki wangu na watu wote milele” kusema kwaheri kila wakati ni ngumu sana, chungu tamu lakini natazama siku za mbele kivinginel, Ahsante HOT97 na la zaidi ni wasikilizaji na leo ndo itakuwa kipindi changu cha mwisho, endelea kusikiliza..Love, Angie…Alisema Angie hewani akiaga wasikilizaji”
Hayo Ndio Maneno Magumu Ya Kwaheri Aliyoyasema Angie wakati anaaga fani hiyo aliyoifanya katika kampuni hiyo katika kipindi cha miaka 25, ameacha kazi akiwa na umri wa miaka 43 ana mtoto anaitwa Niko Ruffin.
Angie amezaliwa tarehe 9 Januari 1971,
Angie Martinez (kulia) akiwa na Jay z ndani ya studio za Hot 97 New York.
Katika maisha yake ya utangazaji ameshafanya mahojiano na wasanii wengi maarufu duniani akiwemo marehemu Tupac na Jay Z, alisema mahojiano ya Tupac ilibidi atumue muda mrefu kuhariri kutokana na kile alichokuwa akiongea Tupac ilibidi vitu vingine aviseme ili ieleweke alichokuwa akitaka kusema Tupac” alisema Angie