Laveda mshiriki mtanzania wa shindano la big brother Africa hot Shorts ndiye aliyeukwaa uongozi wa nyumba katika wiki ya kwanza baada ya mashindano hayo kuzindliwa rasmi leo jumapili october 5
Laveda amepata ushindi huo baada ya kuangoza kwa kura 85% za ushindi wakati anaonyesha kipaji chake cha kupuliza saxophone ikiwa ni style mpaya ya kaka mkbwa kuwaingiza wa shiriki kwa namna ya kila mmoja kuonyesha kipaji chake,
Mtanzania Mwingine Idriss alishika nafasi ya tatu kwa 62%kwa kuonyesha kipaji cha kucheza jukwaania huku mkenya sabina akichukua point 72% kwa ku chekesha watu (comedy)
maana yake ni kwamba watanzania tunauhakika wa kuwa safe ndani ya nyumba kwa wiki zaidi kutokana na cheo hicho ambacho kwa kawaida mkuu wa nyumba anauwezo wa kumtoa mtu kafara na kumsave mwingine matumaini ni kumsave mtanzania mwenzia kama naye kura hazitamuelemea kwasababu kwa mapema watu wanakuwa hawajajuana bado na kinachofuata ni kupigiana kura kwa kukumbuka majina tu
Msanii Kutoka Tanzania Diamond Platinum alikuwa moja ya watumbuizaji usiku huo, washiriki ni 25 na mshinda atakayebaki wa mwisho aktika nyumba atazawadiwa kiasi cha dola za kimarekani 300,000 huku siku za kuishi ndani ya jumba hilo zikiwa zimepunguzwa hadi kufikia 63 badala ya 90 kama ilivyokuwa
siku za nyuma