Mtoto Mdogo wa kiume Jaxon Taylor mwenye umri wa miezi 11 amefariki Dunia baada ya familia yake kumsahau ndani ya Gari kwa takribani zaidi ya saa mbili joto lilipozidi na kuwa 78c siku ya jumamosi walipokuwa wanarejea toka kanisani
Familia ya mtoto huyo akiwemo babu yake shangazi yake na mjukuu mwingine walirejea nyumbani kutoka kanisani huko Georgia mida ya saa 3pm. hakuna aliyekumbumka kumuingiza Jaxon ndani ya nyumba toka garini
Familia hiyo iligundua tu kumsahau mtoto garini mara baada ya mama yake mzazi anayefanya kazi ya uuguzi usiku kucha kuamka mida ya 5.30pm na kumuulizia mwanae
“Imeonekana walikuwa na mawzo mengine kichwani” Walker County Sheriff Steve Wilson Wilson alikiambia kituo cha matangazo cha CNN.
“Kulikuwa na uhaba wa mawasiliano kati ya wale watu wazima watatu waliokuwemo. kila mmoja alidhani mwenzie alishamchukua mtoto na kumpeleka ndani na kumlaza , hawakuwasiliana nani alimchukua mtoto”
Mtoto Jaxon alikimbizwa hospital lakini iligundulika alishafariki dunia .
Mwanamke huyo aliyevunjika moyo kwa kupoteza mtoto wake wa pekee alishare picha ya mcumba wake na mtoto wake aliyefariki na kuandika maneno yakuchoma
aliandika
“My fiancées family has traveled from out of town to support and comfort us, to force us to eat, drink and move when we would lay in bed and cry.
“My fiancée and I had to leave a restaurant in tears last night when the table next to us had a little girl celebrating her first birthday.”