
Wanasayansi wa Chuo kikuu cha Mississippi Medical Center cha nchini Marekani amekiambia chombo cha habari cha CNN kuwa mtoto aliezaliwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi Amepona baada ya kumpatia matibabu kwa mwaka sasa na kwamba baada ya kumfanyia vipimo anaonekana kupona kabisa. Mtoto huyo alipata maambukizi toka kwa mama yake ambae hakujua kama anavirusi vya ukimwi mpaka siku alioenda kujifungua Hata hivo Dr. Hannan Gay alisema hawakupata nafasi ya kumtibu mama ili kumuepusha mtoto na maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto jambo ambalo ndio lilikua la muhimu kuliko matibabu baada ya tukio kujitokeza. Madaktari wanaomfanyia uchunguzi mtoto huyo wanamatumaini makubwa kuwa amepona na kwamba wanaamini hakuna tena virusi vitakavyojitokeza mbeleni Ndo kusema dawa imepatikana eeh.
