Edinho, mtoto wa Pele amehukumiwa kifungo cha miaka 33 jela.
Kwa mujibu wa BBC, Edinho mwenye umri wa miaka 43, amepewa hukumu hiyo kwa kosa la ulanguzi wa fedha kwa ajili ya kusafirisha dawa za kulevya.
Alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na kutumikia kifungo jela kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya na kujihusisha na genge la wahalifu.
Aliwahi kuichezea klabu ya Santos katika miaka ya 1990, kama golikipa.
Kwa sasa anafanya kazi kama kocha wa makipa wa Santos.
Amekiri kuwa ni ‘mteja’ wa dawa za kulevya, lakini amekanusha kuhusika na uuzaji wake.
Anatarajiwa kukata rufaa.