Mtu mwenye umri wa miaka 53 anayeitwa Mcglynn amemtishia Rihanna kwa kumtumia barua sehemu anayoishi.Mtu huyo kutoka New York alikamatwa Alhamisi 24 kwa kumsumbua mwanadada huyo, Kevin anahistoria hiyo na ameshawahi kukamatwa mara 12 taarifa za NY Daily News zilieleza.
Barua zilitumwa kwa Rihanna kupitia sanduku lake la posta huko California, Kevin alikuwa akifikisha mwenyewe barua za vitisho kwa msanii huyo kupitia mfanyakazi wa Apartment anayoishi Rihanna.
Taarifa za Dail News zinasema kwamba mtu huyo alionekana kwenye video ya security ya jengo hilo katika matukio matatu tofauti katika mwezi wa Julai. Mwezi Julai 8 Kevin alitembelea Lafayette St. Building anapoishia Rihanna. Mwezi Julai 11 alienda mara ya tatu kabla hajakamatwa wiki iliyoisha baada ya kukuta wakielekezwa kwenye jina lake na address.
Mtuhumiwa huyo kupitia barua zake alikuwa akilalamika akirudia kwa muita Rihanna b..ch na kumtishia Rihanna kwenda kwenye apartment yake.
Msaidizi wa mwasheria wa mahakama James Vinocura iliripotiwa akielezea barua hizo kwa jaji wa mahakama, “Uhalisi wa barua hizo zinachanganya, zote zinaelezea mahusiano, kama nilivyozionyesha kabla, hiyo kweli hakuna” alisema.
Katika malalamiko yake Mcglynn yalieleza kwamba Rihanna pia na Jay Z na Kanye West walimuibia materials yake, kwa sasa bwana huyo amekamatwa na hakuna zamana kwa uamuzi wa Jaji Abraham Clott.