Muimbaji wa ngoma kali inayoitwa No Love remix akiwa na Nicki Minaj alianguka akiwa hajijui katikati wakati wa show yake usiku wa Jumapili huko katika jiji la New York na watu wakutoa huduma ya kwanza walifika haraka kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza.
Mshindi huyo wa tunzo ya BET ya msanii bora wa mwaka alionekana kuzimia wakati wa show yake katika ukumbi wa Irving Plaza downtown Manhattan, August alikuwa akitembea pembezoni mwa stage ambapo ghafla aliangukia umati wa mashabiki.
Mashuhuda wameiambia TMZ……mshikaji alionekana kutulia baada ya kuanguka ndipo walinzi wakamfuata akiwa katikati ya mashabiki na haraka wakamchukua kumpeleka backstage.
Watoa huduma walionekana wakiingia katika eneo la tukio kwa ajili ya matibabu kwa muimbaji huyo.
Ngoma kali za August ni Ghetto akiwa na Rich Homie Quan.
Mashuhuda wanasema August alibebwa kwenye machela, lakini ilikuwa ikitazamwa sana kuwapungia mashabiki wakati akitolewa nje, na mpaka sasa haijulikani hali yake inavyoendelea, simu zimejaribu kupigwa kufuatilia anaendeleaje lakini hakuna majibu.
Tukipata taarifa jinsi August anavyoendelea hapa hapa kupitia salmamsangi.com tutakuhabarisha, kwani ndo zetu kukupatia infos za uhakika.