NMB ikiwa ni benki ya chaguo la watanzania wengi,sasa basi taarifa
njema ni kwamba (14 Sept) imezindua rasmi kampeni kabambe ‘Weka na
Ushinde’ ambayo itakushawishi wewe mteja kuweka fedha benki ili uweze
kujipatia ushindi ambao si wa Bajaji,Bodaboda,Baiskeli au fulana za
NMB tu bali pia faida kubwa ya riba na usalama wa pesa zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika
uzinduzi huo Meneja wa Amana za wateja katika benki hiyo Bw.Boma
Raballa amesema kwamba kampeni hiyo itafanyika katika kipindi cha
miezi mitatu kuanzi sasa mpaka Desemba 29,2014
Zawadi hizo zinathamani ya zaidi ya TZS 500 Milioni ambazo ni
(Bajaji-52,Bodaboda-52,Baiskeli-400 na fulana-500).