Leo ni mwaka mmoja tangu Msanii wa filamu nchini Steven Kanumba atutoke.
Marehemu Steven kanunba ataendelea kukumbukwa kutokana na mchango wake mkubwa kukuza sanaa ya filam hapa nchini, pia kutokana na umahiri wake aliokua nao katika swala zima la Uigizaji.
Marehemu Kanumba aliwainua wengi sana ambao nao kwa sasa wanamafanikio makubwa katika fani hii ya sanaa ya filam akiwemo Wema Sepetu Ambae kamwe hasiti kumshukuru kanumba kila apatapo nafasi ya kuongea.
Kanumba alifariki siku kama ya leo mwaka 2012 japo kwa mwaka huo tarehe hii ilidondokea usiku wa Ijumaa Kuu ya kuelekea Pasaka.
Kanumba alifariki nyumbani kwake sinza jijini Dar Es Salaam baada ya kuanguka ikiwa inasemekana alisukumwa na mpenzi wake Lulu ambae pia ni mcheza filam nchini katika ugomvi wa mapenzi uliokua unaendelea.
Kanumba alizikwa katika makaburi ya kinondoni na mazishi yake kutajwa kuvunja rekodi kwa kuzikwa na watu wengi baada ya Yale ya Mwl.Nyerere.
Roho yako ipumzike kwa Amani. Utakumbukwa Daina.