Afrobeat king,
Femi Kuti amesema amegundua kwamba watoto wawili kati ya watoto wake wote watano aliokua anadhani ni wake kumbe sio wake
Kwenye Mahojiano na Jarida la IEncomium , Femi amesema vipimo ya vinasaba DNA vimetoa majibu kuwa watoto wawili wakike na wakiume kati ya watoto wake watano waliopewa majina ya Tosin na Dupe ambao walizaliwa baada ya Mtoto Kifungua mimba chake , Made, sio wakwakwe wa kuwazaa ‘biological father’.
“Nilifanya Vipimo vya vinasaba DNA test na nikaambiwa kati ya watoto wote watano wawili si wangu wa kuwazaa, wawili wa mwanzo baada ya kijana wangu wa kwanza Made wakike na kiume, Ni kweli kabisa sijawahi kufikiri mtu anaweza kukupa kitu ambacho si chake, ninawatoto wa kiume watatu tu sasa kwa uhakika, Siwezi kuwa baba wa watoto ambao nilifanyiwa tu mchezo niamini ni wangu,” Alisema