Mwanamuziki Ray C aliyewahi kuathirika na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya amesherehekea Mwaka Mmoja tarehe 8/11 Tangu Afanikiwe kuacha kutumia madawa hayo kwa msaada wa hospital ya mwananyamala kitengo cha kuhudumia waadhirika wa matumizi wa madawa hayo kwa kupata dozz maalum inayosaidia kuweza kuachana na matumizi ya madawa hayo.
Ray C ametupia picha kadhaa mtandaoni akiwa na wenzake waliofanikiwa kwa pamojakutimiza mwaka mmoja bila matumizi ya maawa mabaya ya kulevya
Ray c aliandika katika picha hii
“Nawapenda sana hawa wenzangu wote tulioligundua tatizo na sasa tumepona na tunamshukuru Mungu, Tanzania Bila Ukimwi Inawezekana”