
Watu 298 wamefariki katika ajali iliyotokea jana Alhamisi 17 wakati ndege ya Malaysia MH17 ilipolipuliwa kwa bomu na magaidi.
Kati ya watu waliokufa, watoto ni 80 wakiwemo watoto watatu Wakiaustarlia ambao walikuwa wakisafiri na babu yao Nick Morris.
Taarifa za gazeti moja la Austarlia zinasema familia hiyo ilikuwa katika mapumziko na wazazi wao, wazazi wao walibaki Amsterdam wakiendelea na mapumziko kwa siku chache zaidi, wakati Bwana Norris aliwachukua wajukuu zake kwa ajili ya kurudi Austaralia walikuwa wakitakiwa kurudi shuleni.
Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Kuala Lumpur kwenda Austarali.
Zaidi ya watafiti 100 wa kutoa misaada ambao walikuwa wakielekea kwenye mkutano wa kimataifa huko Australia wakitokea Uholanzi walikuwepo kwenye ndege hiyo.
Kulikuwa kuna abiria 173 wa Uholanzi, 27 wa Australia, 44 wa Malaysia, 12 wa Indonesia, 9 wa Uingereza, 4 wa Ubelgiji, 4 wa Ujerumani, 3 wa Philippines, 1 wa Canada na New Zealand.
