
Ndege nyingine iliyokuwa inasafiri kutoka Nigeria Kwenda Gabon ikipitia Cameroon Imeripotiwa kupotea
Ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni moja ya KiMarekani, Global Aviation iliondoka Uwanja Wa ndege wa Kano Huko Nigeria mida ya Saa 12 jioni Jumatatu ya may 23 na ilitarajiwa kutua uwanja wa ndege wa Doyla Cameroon kabla haijaendelea na safari mpaka Gabon ambapo ilitarajiwa kufika mida ya saa 11pm ambapo haikufika kama ilivyotarajiwa,
Vyombo Vya Usalama Cameroon vimesema ndani ya ndege palikuwa na Rubani Mmoja Tu Mmarekani
Taarifa zaidi kutoka Cameroon zimesema Mawasiliana ya mwisho waliofanya na ndege hiyo ni wakati ipo sehemu inaitwa Mango mda wa kama masaa mawili kutoka Cameroon
Mpaka sasa hapana taarifa za kuonekana kwa ndege hiyo japo uchunguzi bado unaendelea
