Taarifa za CNN Ndege hiyo ya shirika la Algeria, vyombo vya usalama vimethibitisha kwamba ndege hiyo iliyokuwa na wati 116 iliyokuwa ikitokea Burkina Faso ilianguka kaskazini mwa Mali.
Shirika hilo limesema iliangukia katika eneo la Tilemsi karibu kilmita 70 kutoka kusini mwa Gao.
Uwanja wa ndege wa Ouagadougou umetoa maelezo kupitia tovuti yake kwamba majeshi ya Ufaransa yalienda katika eneo hilo na kukuta mabaki ya ndege hiyo kati ya zgao na miji miwili ya Kidal katika ukanda wa jangwa ambapo ni vigumu kufika.
Kufikishwa kwa misaada ya madawa na usalama katika eneo hilo inachukua siku nzima.
Abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo ni raia 51 wa Ufaransa, 27 wa Burkina Faso, 8 wa Lebanon, 6 wa Algeria, 5 wa Canada, 4 wa Ujerumani, 2 wa Luxembourg, 1 wa Uswiss na wafanyakazi 6 raia wa Hispania.
Tuwaombe majeruhi katika ajali hiyo Mungu awaponye na warudi katika hali zao za kawaida.