Ndege ya shirika la ndege la British Airways iliwaka moto jana wakati inajiandaa kupaa katika uwanja wa ndege huko Las Vegas Marekani
Kwa Mujibu wa ripoti Ndege hiyo Boeing 777 ilikuwa tayari kuruka kwenda uwanja wa ndege wa London’s Gatwick,
hata hivyo kabla ya kuruka abiria walisikia kishindo kikubwa na baada ya dakika moja rubani aliwatangazia abiria ya kuwa kuna dharura na itabidi Wawaondoe Abiria ndani ya ndege hiyo
Uzuri ni kwamba hakuna kifo wala majeruhi, Chanzo Cha Moto Huo Bado Hakijawekwa wazi