
Ndovu Special Malt kwa mara nyingine imefanya sehemu nyingine ya kitu kizuuuuri kinachofahamika kama Ndovu Spotlight Studio ndani ya Hotel ya JB Belmont usiku wa jana Alhamisi 21 Agosti 2014.
(Ndovu Spotlight Studio)
Waliong’aa na kushiriki ndani ya studio ya Ndovu Spotlight siku ya jana usiku ni mchekeshaji maarufu nchini Tanzania kupitia kipindi cha Vuvuzela kinachoandaliwa na Vuvuzela Entertainment na kurushwa kupitia Clouds TV, pia ni mtangazaji wa redio ya Choice FM 102.6 Dar es salaam.
(Evans Bukuku Mchekeshaji na Mtangazaji wa Choice FM)
Mwingine aliyeshiriki katika studio za Ndovu Spotlight jana ni mjasiria mali, mpiganaji Mercy Kitomari mwanzilishi wa Newlas Gelato. Na wa mwisho alikuwa Andru Mahiga – Mbunifu na Mkurugenzi wa Maanisha.
(Andru Mahiga – Mbunifu na Mkurugenzi wa Maanisha)
(Mwanzilishi wa Newlas GelatoMercy Kitomari)
Watu 150 walioshiriki katika Ndovu Spotlight Studio walipata nafasi ya kuwauliza maswali The (spotlighters) waliokuwemo siku ya jana kuhusu uzoefu wao na changamoto mbalimbali walizokutana nazo wakati wakipigania kufika walipo na kutimiza ndoto zao.
(Mtangazaji wa Ndovu Spolight Studio)
Ndovu Speal Malt (NSM) ilianzisha wazo la Spotlight kama njia moja wapo ya kutambua na kusherekea mafanikio ya vijana wa Kitanzania waliofanikiwa katika mambo mbalimbali katika maisha kwa njia moja au nyingine. Kukiwa na simulizi za kuvutia na ambazo zitamfanya mtu asikate tama toka pale alipo azidi kujituma zaidi kwani katika maisha ya kutafuta mafanikio kuna changamoto nyingi.
(Washiriki wakisikiliza kwa makini)
Kwa kuwatumia washiriki wa spotlight wakiwa ni vijana wa Kitanzania waliofanikiwa, kila mmoja alielezea simulizi yake katika maisha yake jinsi alivyoanza changamoto mbalimbali na pia kuwatia moyo vijana wenzao wa Kitanzania katika kila wanachokifanya.
Inasemekana vijana wengi wanapenda sana kuanzisha vitu au kuanza kitu kikiwa kikubwa au na mitaji mikubwa na kusahau inatakiwa uanze na kidogo taratibu kikikuwa siku baada ya siku, kujituma zaidi kutafuta network zaidi badala ya kukaa na kusubiri.
Unapokuwa na wazo, wazo haliwezi kuwa pesa mpaka utoke ulipo ukatafuta watu ambao wanaweza kukusaidia na kukuunganisha na watu wengine ambao wanauzoefu na vitu kama hivyo.
Mafanikio, malengo na kuendelea na safari ya kutafuta ndoto yako, kama hauna mtaji unaweza kujibrand wewe kwanza kwenye kile unachokifanya, penda unachokifanya, kifanye kwa usahihi na kwa ubora mkubwa huku ukijiamini na kushindana na bidhaa za kimataifa uukilinganisha na kile unachokifanya.
(Watu mbalimbali wakiuliza maswali kwenda kwa spotlighters)
Ukiangalia watu wengi waliofanikiwa walianza na kidogo, chini lakini walikuwa na malengo huku wakifanya wanachokifanya kwa bidii bila kuogopa watu watakuonaje, kwa sababu wakati unaanza watu watakucheka wataona kama mwendawazimu lakini kama unajitambua na unapenda unachokifanya kikiwa katika ubora ambao mtu yeyote anaweza akakipenda hiyo ni njia moja wapo ya kufanikiwa katika maisha na kutimiza ndoto yako.
(Good time)
Ndovu Special Malt ni bidhaa inaaminiwa na inashindana na bidhaa za kimataifa na kushinda, kwa muda wa miaka minne Ndovu Speal Malt imeshinda tuzo za Gold na Grand Gold kupitia Monde Selection Committee huko Geneva kwa kuwa ni bia inayopikwa kwa muda mrefu ikizingatia ubora wa kimataifa kwa kuwa na ladha nzuri.
Kupitia tuzo mbalimbali za Gold ambazo Ndovu Special Malt imeshinda, Ndovu imeonyesha na kuthibitisha kwamba Mtanzania katika sehemu ya ubora duniani, kama walivyo washiriki wa Ndovu Spotlight Studio kwamba wao ni Watanzania ambao wana uwezo na ubora wa soko la kimataifa kupitia yale wanayoyafanya.
