
Baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutangaza kuifungia kampuni inayoongozwa na Mkurugenzi wake ambae ni Hashim Lundenga kampuni inayojulikana kama Lino International .
Kusimama kufanya shindano la Miss Tanzania kwa muda wa miaka miwili, Mkurugenzi wa kampuni hiyo ameibuka na kutoa kauli akisema hatua hiyo imefaikiwa kutokana na watu wasio na nia nzuri na shindano la urembo nchini ambao wanataka kutoa katika mstari shindano hilo hapa nchini.
Lundenga amesema “ Uamuzi wa BASATA ni utekelezaji wa dhamira ya wachache walioamua kuhakikisha Miss Tanzania inapotea kwenye ramani ya burudani nchini”
