
Mmiliki wa Kimarekani wa sehemu ya wanyama (Mexico Wildlife Center) ameuliwa na ngamia baada ya kutoka sehemu aliyokuwa amefungiwa, Richard Mileski mwenye umri wa miaka 60 alikuwa akitembea sehemu ya ngedere ndipo mnyama huyo alipotoroka na kumburuza chini na kuanza kumkanyaga, kabla ya kumng’ata ng’ata na kumkalia juu yake.
Ingawa na juhudu zote zilizofanywa na wafanyakazi waliokuwa wameshtushwa sana na tukio hilo, Bwana Mileski alikufa papo hapo.
Taarifa za Mailonline, Antonio Gomez, mzungumzaji wa huduma ya dharura wa eneo hilo aisema walipofika watu walisema kwamba ngamia ametoka eneo lake na amempiga mtu, amemburuza, amemkanyagakanyaga, amemng’ata, amempiga na amemkalia.
Mfanyakazi wa Park hiyo alikuwa upande mwingine wa park hiyo ndipo alipomsikia Bwana Mileski akipiga kelele kuomba msaada, alikimbia kwenda katika eneo hilo na alijaribu kumpiga ngamia huyo na fimbo.
Walitakiwa wamfumfunge kamba shingoni ili tumvute kwa kutumia gari aina ya pick up ili kumuondoa.
Alikuwa akimhudumia ngamia huyo kwa miaka 15 iliyopita.
