Wakati wewe ulikuwa ukigonga cheers na kula pilau, nyama choma na mambo mengine katika kusherekea siku kuu ya Krisimasi tarehe 25 Desemba 2014,Bahati msanii kutoka Kenya ambaye alishawahi kuja Tanzania na kufanyiwa mahojiano katika kipindi cha Dala Dala Beatz ya Magic FM, alikuja Tanzania akiwa ametoa ngoma yake ya kwanza, pia kabla ya kuwa mwanamuziki alikuwa ni chokoraa (Kapurwa mtoto wa mtahani).
Katika kuendelea kufanya muziki na kukumbuka matatizo aliyopitia siku za nyuma kabla ya kuwa mwanamuziki, Bahati aliwatembelea na kushinda na watoto wasoijiweza katika kituo cha D.C.M. Watoto wote hawa wote aliokuwa nao wanatokea sehemu inaitwa Kayole ndani ya eneo la Estland.
Kevin Bahati alisema anampango wa kujenga nyumba ambayo wataishi watoto hao, msanii huyo wa muziki wa injili Bahati, amesema kwamba anafanya project hiyo kuwasaidia wazazi ambao wana watoto wenye ulemavu kupata sehemu ambazo watapata matibabu maalum kutoka kwa madaktari wenye taaluma hiyo.
Muda sio mrefu naamini Mungu atatoa nyumba maalum kwa ajili ya watoto hawa kwa ajili ya kupata eneo kubwa zaidi. Alisema kwa kusema Team Bahati keep praying for this.