
YMCMB Signee Busta Rhymes amesema siku hizi kuna kitu kimekosekana katika nyimbo kwani nyingi zinafanana.
“Kila mmoja anataka muziki wake ufanane na mwingine tofauti na miaka ya 1990 ulikuwa ukisikia ngoma Fulani moja kwa moja unajua huyu ni nani lakini sasa hivi muziki unafanana sana.Hata ukiingia club siku hizi ngoma zote zinafana huwuzi jua ipi ni ipi nani ni nani zote zinafanana”
Busta Rhymes alisema hayo wakati akipiga stories na XXL nchini Marekani, Kwa sasa Busta Rhymes ameachia ngoma inayoitwa Calm Down ngoma ambayo ameshirikishwa Eminem na pia alifunguka kuwa ngoma hiyo imemixiwa na Eminem.
