Katika watu waliokuwa wakimpa wakati mgumu Oscar Pistorious ni mama yake mzazi wa mpenzi wake Reeva Steenkamp, katika kesi moja iliyoitwa siku za nyuma Oscar Pistorious alilia lakini mama yake Reeva hakumuonea huruma zaidi ya kumwambia muone kwanza hata aibu hana analia unafki.
Lakini hatimaye mama huyo amesema amemsamehe Oscar Pistorious ingawa bado anataka kujua ukweli aliiambia Hello Magazine. “Simchukii Oscar, nimemsamehe, nanatakiwa kufanya hivyo kutokana na dini yangu, lakini nikiwa imara nimuone nanamtetea binti yangu, ni muhimu kwake kujua kwamba nipo kama mama niliyemzaa Reeva na kumpenda, nahisi uwepo wake kila wakati nakuongea nae muda wote.
Naamini kwamba Mungu atasaidia tujue ukweli na sheria itachukua mkondo wake tunachotaka ni kujua ukweli.” Alisema mama yake marehemu Reeva.
Oscar amerudishwa kuendelea kusikilizwa kesi yake baada ya mwezi mmoja wa kuchunguzwa akili na kama akikutwa na kosa atafungwa kifungo cha maisha jela au atafungwa miaka 15 kutokana na kosa hilo.