
Kumetokea Ajali Ya Helkopta Leo Mida ya Asubuhi Katika uwanja Wa Ndege Wa Ndege Dar Es Salaam Ambapo Viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick na kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova walianguka na Helikopta hii asubuhi ya April 13 2014 kwenye uwanja wa ndege Dar.
Hitilafu ilisababisha helikopta kuanguka wakati ikipaa kuwapeleka kwenye maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo hata hivyo walinusurika kifo isipokua majeraha madogomadogo tu.
Hata Hivyo Hiy0 Haikuwa Sababu ya viongozi haoi kukatisha ziara yao hiyo ya kutembelea maeneo yaliothirika na Mafuriko yalioikumbwa Jiji la Dar Es Salaama na Maeneo Mengine
Baada ya kujiona wapo fiti baada ya Ajali hiyo isipokuwa majeraha madogo madogo tu Viongozi hao waliingia ndani ya magari yao na kutumia usafiri wa magari kuwafikisha katika maeneo waliyopanga kuyatembelea kama inavyoonekana katika Picha
