
Wikiendi iliyopita ilishuhudia kilele cha kampeni ya Lite Up The Weekend ambayo iliyoendeshwa na bia ya Castle Lite huku ikihusisha wanywaji wa bia hiyo waliopata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kwa kutuma namba za ndani ya kizibo. Katika siku hiyo washindi wa droo kubwa walipata nafasi ya kukutana na kujumuika katika Yacht Party iliyoanzia katika ya hoteli ya Coral Beach kabla ya kupanda Yacht iliyowapeleka katika kisiwa cha Mbudya. Baadhi ya wapenzi wa bia ya Castle Lite katika picha ya pamoja mara baada ya kukutana hoteli ya Coral Beach siku ya Ijumaa
Ndani ya Yacht tayari kwa kuanza kufurahia mandhari ya bahari ya Hindi
Pozi
la picha ya ukumbusho katika Yacht Hali ya hewa iliruhusu wote kufurahia uwepo wao katika tukio hili
Hakuna Party bila selfie kama wanavyoonyesha wawili hawa
Safari ikaishia katika kisiwa cha Mbudya ambako walishuka kuburudika
Mpira wa miguu ufukweni ni raha kwa kila mtu bila kujali jinsia
Stori za hapa na pale mara baada ya kurejea hoteli ya Coral Beach
Castle Lite ikiendelea kuwaburudisha
