Polisi Visiwani Zanzibar wamethibitisha kutokea milipuko miwili ya mabomu Jumatatu leo mchana visiwani humo.
Mkuu wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame amesema milipuko miwili imetokea leo katika eneo la mgahawa wa Mercury huku mlipuko mwingine ukiwa umetokea katika eneo la Mkunazini,Karibu na kanuisa la Aglican
Mkuu huyo wa Polisi Zanzibar amesema kuwa hakuna vifo wala majeruhi katika matukio yote wala mali iliyoharibiwa, isipokuwa madhara ya kisaikolojia kutokana na hofu na taharuki kutokana na matukio hayo.