Hakuna jitihada zisizokua na Manufaa baadaye, mimi na wewe ni shahidi kwa jinsi kijana huyu alivyo muhangaikaji kwa nguvu na juhudi binafsi zaidi ya kuwa ni Muajiriwa ameonekana kufanya kazi yake kwa juhudi binafsi, Pia ukilinganisha na historia yake katika uchakarikaji kulingana na maelezo yake… Hatamae juhudi za kijana huyu zimezua matunda na hii ndio taarifa mpya kutoka katika mtandao wake wa milladayo.com
Hii ilikua ni njiani nikiwa kwenye gari ya polisi kwenda kufata stori kwa Babu wa Loliondo, nililazimika kulipa pesa yangu ya mfukoni kuweka mafuta ili nipelekwe na Polisi kwa sababu katikati ya Msitu kulikua na vita hivyo magari ya kawaida hayakua yanakwenda…… ni moja kati ya ripoti nitakazozikumbuka sana.
“Kwanza nakushukuru mtu wangu wa nguvu kwa kuwepo hapa, pili nawashukuru Maboss wangu wote niliowahi kufanya nao kazi kuanzia TVZ, Wapo Radio, ITV/RadioOne na familia yangu CloudsFM/TV nilipo sasa hivi.Katika mwaka wangu wa nane kwenye hii kazi, ninayofuraha kutangaza leo kwamba Clouds FM imeniwezesha kuonekana na hatimae kuitwa na watu wa Multichoice SOUTH AFRICA kwa ajili ya interview ambayo baadae nilishinda na kuchaguliwa kuwa ripota wao.
Nguvu zangu nyingine sasa hivi nitazielekeza kwa kuandika stori na kurekodi Video za matukio mbalimbali kwa ajili ya kazi yangu mpya nikiwa kama ripota wa DSTV South Africa kuiwakilisha Tanzania.
Nawashukuru wote kwa kuendelea kuwa pamoja na mimi watu wangu wa nguvu, naamini kwa asilimia 100 kwamba support yako inahusika sana kwenye maisha yangu, asante pia kwa familia yangu ya www.facebook.com/millardayo www.twitter.com/millardayo na www.instagram.com/millardayo”
Hivyo ndivyo… Kila la kheri Millad.