Ubalozi wa Uingereza nchini leo umezindua rasmi huduma mpya ya viza za kipaumbele (priority visa service) kwa ajili ya watanzania wanaosafiri kwenda nchini uingereza.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Balozi wa Uingereza nchini bi.Dianna Melrose amesema huduma hiyo mpya ya viza itasaidia kuendeleza uhusiano mzuri ulipo katika ya nchi hizo mbili na kuimarisha biashara ili kuongeza uwekezaji pamoja na kuchangia maendeleo ya Tanzania katika upatikanaji wa ajira kwa watanzania walioko nchini Uingereza.
Bi.Melrose amesema kupitia huduma hiyo mpya, ubalozi utahakikisha maombi ya viza yanafanyiwa kazi ndani ya siku tano kama hakutatokea tatizo lolote upande wa mwombaji ambalo hata hivyo atajulishwa kabla na utoaji wa viza utafuata sheria za kawaida za uhamiaji.