Kwa siku ya pili ikiwa ni harakati za kupata katiba mpya tangu jeshi la nchi hiyo kuuangusha utawala wa Rais wa zamani Mohammed Morsi.
Jeshi la Misri linashinikiza kura ya ndiyo ili kuhalalisha kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa rais wa Misri Mohamed Morsi, aliyeondolewa madarakani mwezi Julai mwaka 2013.
Vituo vya upigaji kura vimekuwa vikifunguliwa saa tatu asubuhi huku vikosi vya ulinzi vikiimarishwa tangu siku ya Jumanne huku watu tisa wakiripotiwa kuuawa katika vurugu zilizotokea ambapo wengi wa waliouawa ni wafuasi wa Morsi..,huku hali ya usalama ikiwa imedhibitiwa vikali,Katiba mpya ndio itatoa njia kwa uchaguzi mkuu mpya kufanyika.
Madhumuni ya katiba hiyo mpya ni kutupilia mbali katiba ya zamani iliyopitishwa na iliyokuwa serikali ya Mohammed Morsi miezi kadhaa kabla ya jeshi kumuondoa mamlakani.