Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amefikisha miaka 90 Jana Juma tatu na kuwa rais mkongwe zaidi barani Afrika…
Hata hivyo sherehe za siku ya kuzaliwa kwake zitafanyika Jumapili huku kukiwa na tetesi kuhusu hali yake mbaya ya kiafya pamoja na mvutano kuhusu uongozi wa chama tawala…
ambapo Sherehe hizo zinakisiwa kugharimu dola milioni moja.
Rais Mugabe Alizaliwa katika kijiji cha Kutama, kusini-magharibi mwa jiji kuu, alisomeshwa na wayesuti, na baadaye akawa mwalimu kabla kujiingiza katika harakati za kupigania uhuru wa Zimbabwe…
Uwanaharakati wake ulimfanya afungwe gerezani kwa miaka 11, na baadaye mwaka 1980 akawa rais wa kwanza wa Zimbabwe.