Rais wa mpito katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba Panza, ameapishwa katika sherehe maalum mjini Bangui….
Samba Panza, ambaye ni mwanamke wa kwanza kuwahi kutawala nchi hiyo, ameahidi kumaliza ghasia za kidini pamoja na kukabiliana na hali mbaya ya kibinadamu.
Anamrithi Michel Djotodia, aliyetawazwa kama Rais wa kwanza muisilamu nchini humo na waasi wa Seleka waliomsaidia kuingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi.