Kila ifikapo tarehe 14 Februari
kila mwaka sehemu mbalimbali duniani husherekea siku hii ya Valentine, ikiwa ni siku muhimu ya kuonyesha upendo kwa yule umpendae au wale uwapendao, awe mpenzi wako, kaka yako, mama yako, dada yako, baba, shangazi, mama mdogo, rafiki na watu wengine. Kupeana zawadi mbalimbali nzuri kubwa au ndogo ya kitu chochote kile, kwenda out inategemea una vibe gani, unaweza hata mkachill home lakin lakini mkafanya vitu tofauti siku hii, hata chakula kinakuwa tofauti kidogo kwa sababu ni siku muhimu kwa kuonyesha upendo kwa wale tunaowafeel. Hii ni siku muhimu sana kwa watu kuonyesha upendo, kama ulikuwa mmekosana na mtu nadhani huu ndo muda wakusameheana na kuanza maisha mapya, kwa sababu kuna msemo unasema “No body’s perfect” unaweza ukawa umemkosea mtu au amekukosea huu ndo wakati mzuri wa kumwambia akusamehe na unampenda. Siku hii isitumike ndo siku ya kutafuta michepuko, Siku ya Valentine sio siku ya kufanya ngono kama baadhi ya watu wanavyoelewa, ni siku ya kudhihirisha upendo kwa watu wako, ingawa kuonyesha upendo kwa watu tumeagizwa kufanya hivyo siku zote za maisha yetu. Tuwe waangalifu isije ikawa baaada ya Valentine yakaanza majuto, ukajikuta umepata magonjwa ikiwemo virusi vya Ukimwi, gono, kaswende na magoonjwa mengine. Tusherekee vizuri, kama ni wana ndoa huu ndo muda wa kulinawarisha penzi, mnaweza mkaenda sehemu fulani tulivu ingawa sio lazima inategemea na kipato chenu, ila mnaweza hata kushinda nyumbani lakini siku hii inakuwa ni tofauti kidogo, siku ya Wapendanao mnakaa mnapanga maisha yenu katika siku zijazo. Salmamsangi.com inawatakia “Happy Valentine Day”